Wacha tukomeshe ujauzito wa mapema na usiotarajiwa katika Afrika Mashariki na Kusini
Fikiria kanda la Afrika Mashariki na Kusini ambapo vijana wote wamewezeshwa na wana maarifa, maelezo, uwakala na msaada ili kuzuia ujauzito wa mapema na usiotarajiwa na kufikia uwezo wao kamili.
Sheila anazungumza kuhusu sera za kibaguzi na athari zao mbaya kwa vijana ambao wanapata EUP, na jinsi wanaweza kuzuiwa kupitia mabadiliko ya sera na kuboresha upatikanaji wa huduma za CSE na SRH.
Ilda anazungumza kuhusu kuwashirikisha wazazi na jamii katika mchakato wa kufanya uamuzi wa utekelezaji wa sera za CSE na SRH, na jinsi hii inasababisha sera bora na zinazotekelezeka za kuzuia EUP na kuingia upya shuleni.
Peris anazungumza kuhusu jinsi elimu kamili ya ujinsia na mawasiliano wazi yatalinda afya ya wanafunzi, kupunguza viwango vya ujauzito wa mapema, na kuwaweka shuleni.
Rudo anazungumzia kuhusu kuwaonyesha watoto wako kuwa unajali ustawi wao kwa kuzungumza nao juu ya vitu vinavyoathiri afya yao--Ikiwa ni pamoja na ngono.
Bafana anazungumza kuhusu hitaji la kuwashirikisha wanaume na wavulana kwenye mazungumzo juu ya afya ya kijinsia na uzazi, na kufanya kazi katika sekta zote ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu inatimika.
Anazungumzia: Shellsy anazungumza kuhusu kuhamasisha vijana kuchukua udhibiti wa maisha yao ya baadaye kwa kujifunza juu ya ngono salama na machaguo yao ya vizuia-mimba na huduma zingine za SRH.
Jamil anazungumza kuhusu umuhimu wa sera za kuingia upya shuleni kwa wasichana wajawazito na walio na watoto na jinsi wanaweza kufaidi vijana na jamii, ili kusababisha ufukiaji wa juu wa elimu.