Uhamasishaji wa kijamii unaruhusu jamii kuwa tayari kusikia ujumbe wa Kampeni ya Hebu Tuzungumze!. Mkazo unapaswa kuwa juu ya kuchochea mazungumzo, kuwafanya watu wazungumzie matatizo inayowakumba, kushiriki hisia zao na suluhisho juu ya masuala yanayohusiana na EUP, na polepole kupokea maelezo na mabadiliko yanayopendekezwa.

Mwongozo halisi juu ya jinsi ya kutekeleza shughuli za uhamasishaji wa kijamii umejumuishwa hapo chini. Chini ya ukurasa huu utapata nyaraka zinazoweza kupakuliwa na hatua halisi za jinsi ya kufikia vikundi mbali mbali vya hadhira kama wazazi na familia, viongozi wa dini na raia, walimu na waelimishaji na vijana. Tumia miongozo na Zungumza Kuihusu.

KWA NINI UHAMASISHE?

Unajali. Unaweza kuleta mabadiliko!

ASANTE kwa kuwajali wasichana na kwa kusaidia jamii yako!

Kuna wasichana wengi waliobalehe wanaopata ujauzito, ulio na matokeo mabaya kwao, watoto wao na jamii yako nzima. Hebu Tuzungumze! Inafanyika kote nchini na katika kanda, kwa lengo la kuzuia ujauzito wa mapema na usiotarajiwa (EUP).

Asante kwa kujiunga na juhudi hizi kama mhamasishaji wa kijamii!

Fikiria juu ya kile kinachotokea msichana anapokuwa mjamzito akiwa bado shuleni, wakati mwili wake bado haujakomaa. Je, ni sawa kufukuza msichana kutoka shule? Je, ni haki kwake kukabiliwa na matatizo ya kimatibabu yanayoweza kuepukika badala ya kusoma na wenzake? Je, watoto wanapaswa kuwalea watoto?

Kama mshawishi katika jamii yako, una uwezo wa kuleta mabadiliko. Utawasaidia watu kuelewa gharama za EUP na manufaa ya kuiepuka.  Pamoja na wahamasishaji wengine wa kijamii, na kwa usaidizi wa mwongozo huu, utaelimisha na kuhamasisha watu katika jamii yako kugeuza mitazamo na kubadilisha mazoea mabaya ambayo husababisha wasichana kuwa wajawazito kabla ya kuwa tayari.

UNAWEZA KUFANYA NINI ili Kuleta Mabadiliko?

Unaweza kuanza kusambaza maelezo kuhusu EUP mara moja. Kama mhamasishaji wa LTC, utafikia vikundi tofauti vya jamii na viongozi, kupitia vyombo vya habari vilivyopo na rasilimali zinazotolewa na LTC.  Unapoendelea, utawahimiza watu kuwa mabingwa. Unapaswa kusaidia wanaojitolea ili wakusaidie kwa dhamira ya kuelimisha na kutetea kuchukuliwa kwa hatua kupitia mitandao ya kijamii katika jamii.

JINSI YA KUHAMASISHA:

Kama mhamasishaji wa LTC, unaweza kuchukua jukumu muhimu katika kupunguza na hatimaye kuondoa EUP na uharibifu unaosababisha kwa wanawake wachanga na familia zao. Hata hivyo, haitasaidia ikiwa unawaambia watu cha kufanya pekee.  Unahitaji kuwasikiza. Ongea juu ya matatizo yao na maoni yao kwanza na ndipo watu watakuwa tayari zaidi kusikia ujumbe wako.

Pia unataka kuwa mwangalifu juu ya jinsi unavyoongea na kuhamasisha. Unataka ujumbe wako kuingiliana na jamii yako, na kudumu muda mrefu baada ya vipindi vyako kumalizika. Ili kudumisha athari, zingatia zaidi kuwasiliana na watu na kuunda miungano.

Hatua yako ya kwanza ni kubaini watu ambao wana ushawishi katika jamii. Hawa “washawishi wa kijamii” ndio washirika wako wanaowezekana. Wanaweza kuwa mtu yeyote, wa kazi, jinsia, au umri wowote. Wanaweza kuwa viongozi kutoka mashirika ya eneo hilo, wafanyakazi wa afya, walimu wa shule, au viongozi wa kidini. Wanaweza kuwa wazee wa jamii, watu mashuhuri wa eneo hilo, au wanaweza kuwa watu wa kawaida wasio na hadhi rasmi ambao wanajulikana kwa kufanya mambo tu.

Unapaswa kufikiria kwa umakini juu ya mtazamo wa hadhira yako unapopanga mbinu yako ya mikutano ya jamii. Je, ni watu gani ambao unataka wachukue hatua kuzuia EUP? Je, wasiwasi wao ni gani? Mali zao? Unawezaje kuunda mazingira yenye usaidizi ambayo yatawashawishi watu kwamba kuchelewesha ujauzito ni jambo nzuri?

Kama mhamasishaji wa LTC, una nafasi nzuri ya kushawishi uelewa wa jamii yako kuhusu suala hili muhimu, na kuwachochea kutenda.  Kila wakati unapoongea na jirani au kikundi cha jamii, unaweza kuwa mwalimu na mwongozo wao, ukiwasaidia kuelewa jinsi ya kudumisha afya ya familia zao. Mwongozo ufuatao utakusaidia kuwezesha majadiliano madogo, yasiyokuwa rasmi na pia mikutano mikubwa zaidi.

Miongozo ya Mhamasishaji

Mobilisation Guide – Teachers and Educators SWA

. . .

Mobilisation Guide – Religious and Civic Leaders SWA

. . .

Mobilisation Guide – Health Workers SWA

. . .

Mobilisation Guide – Peer Groups and Youth SWA

. . .

Mobilisation Guide – Parents and Families SWA

. . .

Shiriki Kampeni

Kwa habari zaidi juu ya kampeni na anwani hii ya wahusika:
letstalkeup@gmail.com