Kupitia simulizi chanya, Kampeni ya Hebu Tuzungumze! inawaalika watu wa Afrika Mashariki na Kusini kuhusika katika mazungumzo juu ya ujauzito wa mapema na usiotarajiwa.

Kwa kuangazia Mabingwa wa kikanda kampeni inahimiza mazungumzo ya kizazi na uamilishaji wa jamii kama njia ya kukuza mabadiliko katika ngazi zote za jamii, kupitia:

Afya

Kutetea ufikiaji ulioongezeka wa huduma za afya ya uzazi (pamoja na vizuia-mimba) kwa waliobalehe na vijana, bila hukumu au ubaguzi.

Elimu

Kuhakikisha kuwa waliobalehe na vijana wanapata elimu nzuri na ya hali ya juu ya ujinsia ili kuwapa uwezo wa kufanya chaguo sahihi za maisha na kuzuia ujauzito wa mapema na usiotarajiwa.

Haki

Kuhakikisha kuwa waliobalehe na vijana wote wanajua haki zao na wamewezeshwa kufanya maamuzi kuhusu ujinsia, afya na elimu ambayo itawaruhusu kufikia uwezo wao kamili.

Shiriki Kampeni

Kwa habari zaidi juu ya kampeni na anwani hii ya wahusika:
letstalkeup@gmail.com